Sunday, 7 September 2014

SISI PIA NI WANADAMU.

Utamaduni yaani Mila,ni Jadi na Desturi za Kundi la Jamii fulani. 
Mila za Makabila hapa Kenya na hata Nchi zote za Dunia,hasa hapa Afrika, Mwanamke amewekwa baada ya Mwanaume.Swali ambalo Wanawake hujiuliza ni: ''Nani aliyetuweka baada ya wanaume hawa?''.

Kwa kuwaza na kuwazua....kweli hatuwezi tukapata jibu mwafaka.Lakini tunavyojua Mwanaume hujitetea kuwa katika uumbaji wa Binadamu,Mola alimuumba Mwanamke kutoka kwa ubavu wa Mwanaume.Sawa! hatukatai, lakini wanaume wamebadilisha maneno haya nakuongezea yao...''Ati wewe Mwanamke ulitoka kwa ubavu wangu kwa hivyo wewe ni mali yangu,pia niko na haki ya kukufanyia kitu chochote..''.Bado anaendelea,''Naeza kukwadhibu,Unafaa kunizalia hadi nitosheke..kwa sababu wewe ni ubavu Wangu!''. Lo! Jambo hili   ni Upuzi mtupu na Ushindwe.

Haya na turudi kwa mazungumuzo yetu.Nilidhani kuwa Wakoloni walikuja kuvunja Utamaduni kama hizi ambazo kwa wakati huu zimepitwa na wakati..Wanaume watudhibitisha kuwa kila Mwanamke ambaye ana urithi mwingi, anaiba kutoka kwa Mwanamme ama amefanya ushirikina iliapate urithi wote huo.Ukweli ni kuwa sisi wote kama binadamu, Mola alitupa akili SAWA.Hakumpa Mwanamme akili kubwa kuliko Mwanamke ama akampa Mwamamme mkono mzima na Mwanamke akapata nusu.Sisi sote tuko sawa.Wanawake wanastahili kuheshimiwa na wasionekana kama viumbe wa kukaa jikoni pekee,wa kujifungua sana ama wa kupigwa vinyama.
 
 Mwanamke pia ana kibali kutoka kwa Mola.Yeye ndiye aliyepewa kibali cha kuleta uhai hapa duniani jambo ambalo mwanamme hawezi.Ingawa Wanaume hudai kuwa wana nguvu.Kwangu Mwanamke ana nguvu sana kuliko Mwanamme kwa kila kitu kwa mfano nguvu ya mwili hata hisia.Mambo ambayo Wanawake hupitia kwa kweli Wanaume hawawezi vumilia.Kwa mfano,jambo mbaya na nzito likatendeka Wanawake wengi wata jaribu kulitatua na wanafaulu kulitatua.Kwa Wanaume wengi ni heri watoroke ama waliache likiwashinda.Pili,watajaribu kuzungumza na mtu ili awasaidie kulisuluhisha kama Mama,Dada ama Mkewe ambaye pia MWANAMKE.

Basi Wanaume sisi Wanawake ni Watu muhimu kwa maisha yenu Mkubali msikubali hilo ndo ukweli wa mambo.Tafadhali Mwache tabia  duni za kutunyanyasa,kutufanyisha kazi ya sulubu na la mwisho kupiga Wanawake vibaya mnafaa kujua kuwa kila binadamu ana haki ya uhai.Kwani,hata katiba yetu haina ubaguzi wowote.Hakuna mtu dhahabu kuliko mwingine sisi wote tu sawa mbele ya Sheria.SADAKTA.

Mwandisha,
Edith Nene 

No comments:

Post a Comment